Home

NAFASI ZA MASOMO KWA MUHULA UNAOANZA SEPTEMBA 2018

Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania tawi la Singida anawaalika wahitimu wa kidato cha nne na sita kwenye mafunzo ya ngazi ya CHETI (Certificate) na STASHAHADA (Diploma) kwa muhula unaoanza Septemba 2018 kwa kozi zifuatazo:

  1. Menejimenti ya Kumbukumbu (Records Management)
  2. Menejimenti ya Rasilimali watu (Human Resource Management)
  3. Uhazili (Secretarial Studies) - hii ipo ngazi ya Diploma pekee
  4. Utawala wa Umma (Public Administration)
  5. Utawala wa Serikali za Mitaa (Local Government Administration) - hii ipo ngazi ya Diploma pekee
  6. Sheria (Law) - hii ipo ngazi ya Diploma pekee

SIFA YA KUJIUNGA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE)
Cheti cha kumaliza KIDATO CHA NNE chenye angalau UFAULU WA MASOMO MANNE kwa kiwango cha kuanzia D (Hii haijumuishi masomo ya dini)


SIFA YA KUJIUNGA NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA)
Cheti cha kumaliza KIDATO CHA SITA chenye angalau “PRINCIPAL PASSMOJA na “SUBSIDIARYMOJA   AU   Cheti cha msingi  (yaani Basic Technician Certificate) cha kozi inayoshabihiana na kozi unayotaka kusoma toka chuo chochote kinachotambulika na NACTE (ikiambatana na  vigezo vya ufaulu wa D nne kidato cha NNE)


NAMNA YA KUJIUNGA

Kuna njia mbili za kujiunga na chuo, tumia moja tu ya njia hizi:

Moja: Jaza fomu moja kwa moja kwenye Mtandao kwa kubonyeza Hapa

AU

Pili: Jaza fomu inayopatikana kwenye mtandao wetu (www.tpscsingida.ac.tz) ama tembelea tawi letu lililopo Singida mjini, barabara ya kwenda kiwanja cha ndege mkabala na nyumba za polisi ili kupata fomu hiyo, kisha ambatanisha risiti ya benki ya ada ya maombi ya kiasi cha TSh. 10,000 inayolipwa kupitia benki ya CRDB akaunti namba: 0150363185200, yenye jina la akaunti:Chuo cha Utumishi wa Umma Singida, kisha tuma maombi yako kwa: Mkurugenzi, Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Tawi la Singida, S.L.P 1534, Singida, au tuma kupitia anuani yetu ya barua pepe (email address) singida@tpsc.go.tz. Kwa Maelezo zaidi piga simu namba: 0753111560, 0762105177, au 0714906056

Muhimu: Ukijaza fomu ya kwenye mtandao, utalazimika kuambatanisha nakala za vyeti mbalimbali pamoja na risiti ya benki ya malipo ada ya maombi ya shilingi 10,000/= iliyolipwa kwenye akaunti ya benki iliyooneshwa hapo juu

 

MAELEKEZO MENGINE MUHIMU WAKATI WA KURIPOTI CHUONI

Ada ya Chuo

Ada

Kwa Mwaka

Malipo

Muhula wa 1

Muhula wa 2

Muhula wa 3

Muhula wa 4

Ngazi ya Cheti

800,000

400,000

400,000

-

-

Ngazi ya Diploma

1,015,000

515,000

500,000

515,000

500,000

Fomu ya Maombi

10,000

10,000

-

-

-

Kitambulisho

10,000

10,000

-

-

-

 

Sare za Chuo:

Suti ya kiofisi rangi yeyote. Kwa wanaume suruali na wanawake sketi ndefu zinazovuka magoti. Shati la ndani la suti liwe la rangi moja. Kwa wanaume Tai iwe ya rangi yeyote. Viatu viwe vya kiofisi vya rangi yeyote (visiwe vya wazi au raba)

Gharama za Hosteli

Gharama ya hosteli ni shilingi 150,000/=  kwa muhula MMOJA wenye miezi 5 (mwaka mzima una mihula 2).

Viambatanishi Muhimu wakati wa Kuripoti

Unapokuja kuripoti chuoni uje na: Cheti halisi cha kidato cha 4 au hati ya matokeo (result-slip), risiti ya benki ya malipo ya ada ya chuo (ilipwe kupitia benki ya CRDB, jina la akaunti ni Chuo cha Utumishi wa Umma singida, namba 0150363185200, Picha ya rangi ya passport size 1.

Muhimu: Mwanafunzi aje na hela ya kujikimu (chakula na mahitaji mengine) pamoja na kitambulisho mkononi.